Latest Updates & Stories

Home  /  Blog News

HAKI ZA MPANGAJI MWENYE NYUMBA ANAPOVUNJA MKATABA WA UPANGAJI

HAKI ZA MPANGAJI MWENYE NYUMBA ANAPOVUNJA MKATABA WA UPANGAJI

 
  • 693
  • 0
  • 420

Kama mwenye nyumba hajatimiza masharti ya mkataba wa upangaji mpangaji anaweza kufanya yafuatayo- (i) kudai fidia (damages) (ii) kudai mwenye nyumba kutenda vilevile sawa na mkataba (specific performance) (iii) Zuilio kwa amri ya mahakama (injunction) UKARABATI NA MAREKEBISHO YA NYUMBA kwa hali yoyote ambapo mwenye nyumba ameshindwa kufanya ukarabati na matengenezo ya nyumba iwe Salama kwa kuishi kama imeathirika na mafuriko, upepo, kimbunga, tetemeko au moto analazimika kufanya ndani ya siku thelathini, mpangishaji atafanya ukarabati na matengenezo ambayo ni wajibu wa mwenye nyumba kufanya Ikitokea nyumba imeharibika bhasi mpangaji atatakiwa kutuma notisi ya siku 30 kwa mwenye nyumba za kufanya ukarabati. Ikitokea baada ya notisi mwenye nyumba hajafanya ukarabati na hajaomba kuongezewa Muda kufanya marekebisho bhasi ✔ Ikitokea mwenye nyumba ameshindwa kufanya ukarabati Basi mpangaji anaweza fanya ukarabati lakini zile gharama zitafidiwa/katwa na Kodi anayotakiwa alipe kwa mwenye nyumba Mpangaji anaweza kwa hiari yake kama atapenda kufanya tathimini ya gharama za ujenzi na anaweza kufanya marekebisho na atakuwa na haki ya kufidia kupitia kodi Mpangaji akiona mwenye nyumba ameshindwa kufanya ukarabati wa nyumba bhasi anahaki ya kuchukulia mkataba umevunjika na kugoma au kuacha kulipa kodi Haya yote Ni kwa Mujibu wa kifungu 109(2) Cha sheria ya Ardhi No.4 ya Mwaka 1999 Kama ilifanyiwa marejeo Mwaka 2019 Toa maoni yako Share zaidi upate makala zaidi

0 Comments

Hakuna Maoni kwa Sasa

Leave a Comment